
MWANAMUZIKI wa dansi nchini, Johnson Nguza maarufu Papii Kocha amesema amemshangaa mkongwe wa dansi kutoka Congo DR, Koffie Olomide katika wimbo wa Waah alioshirikiana na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platniumz’ kwa kuimba kama rapa.
Akizungumza na paparazi kwenye kiwanja cha kujidai cha Friends Pub kilichopo Sinza, jijini Dar, Papii Kocha amesema amemshangaa Koffie kuimba katika ngoma hiyo kama rapa badala ya muimbaji.
“Mimi nilichomshangaa nnavyomjua Koffi yeye ni muimbaji na siyo rapa lakini katika wimbo huo amefanya kurap.
“Jambo lingine lililonishangaza mimi nilivyosikia wametoa wimbo mpya nilijua kutakuwa na jipya lakini badala yake kumbe ilikuwa ni kuingizia vipande vya wimbo wa Papaa Mobimba na kuufanya wimbo huo uonekane kama remix ya wimbo huo,” alimaliza kusema Papii na kuwapongeza wawili hao kwa ubunifu wao na kunogesha mambo.
STORI: RICHARD BUKOS, RISASI
SOMA HABARI HII KWENYE Gazeti la Risasi bure
SOMA BURE >> RISASI <<
AU
Bonyeza kununua >> RISASI<<
PAKUA GLOBAL APP SASA
-
iOS 👉 https://apple.co/38HjiCx
-
Android 👉 http://bit.ly/38Lluc8