
MWIGIZAJI mkongwe kwenye tasnia ya Bongo Movies, Ahmed Ulotu almaarufu Mzee Chilo amefunguka sababu ya chipukizi kuwabwaga mastaa wakubwa kwenye tuzo za kimataifa za filamu.
Chilo amemtaja Shahista Alidina a.k.a Shaykaa kuwabwaga mastaa wa tasnia hiyo na kutwaa tuzo ya kimataifa nchini Dubai ya World Oscars Signature kwenye kipengele cha Mwigizaji Bora wa kike 2020.
Chilo amewataka wasanii wa tasnia hiyo wanapopata nafasi ya kucheza muvi wajitume na kuonesha uwezo na wasibwete na majina yao tu.
“Unakuta kweli msanii ni staa sasa badala ya kuonesha umahiri kwenye kazi kama lililovyo jina lake unakuta anabweteka na kuzidiwa na andangraundi bila kujijua.
“Sasa huyu msanii amecheza filamu moja tu iitwayo Uhuru na Gharama zake katika nafasi aliyoicheza kama mgonjwa wa akili na kipengele hicho ndiyo kimemtoa na kubeba tuzo hiyo ya kimataifa na kuwaacha mastaa wakibaki na ustaa wao.
“Mastaa tujitume, tuache kubweteka, tutajikuta tunapitwa na wakati,” anasema Mzee Chilo.
STORI; RICHARD BUKOS, DAR