×

Saido Agomea Hoteli Zanzibar

NASEMEKANA kuwa baadhi ya mastaa wa Yanga wamegomea hoteli maalum waliyoandaliwa na waandaaji wa michuano ya Kombe la Mapinduzi.

 

Hiyo ikiwa dakika chache tangu kikosi cha timu hiyo kitue Unguja, Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Jumhuri FC uliotarajiwa kupigwa Uwanja wa Amaan, visiwani humo saa 2:15 usiku, jana.

 

Mastaa wa Yanga ni Saidi Ntibazonkiza ‘Saidoo’, Carlos Fernandez ‘Carlinhos’, Tuisila Kisinda, Mukoko Tonome, Michael Sarpong na Yacouba ‘Songne’.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano kutoka ndani ya Benchi la Ufundi la Yanga, viongozi nao waliungana na wachezaji hao.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa sababu ya kukataa hoteli hiyo ni kutokuwa na hadhi ambapo haijatumika tangu janga la Corona lilipovamia hapa nchini, hivyo mazingira siyo rafiki kwa matumizi ya binadamu.

 

Aliongeza kuwa mara baada ya kugoma, haraka waandaaji wa michuano hiyo wakawabadilishia hoteli Yanga.“

 

Waandaaji walishindwa kuitofautisha Yanga na klabu nyingine shiriki, awali waliwaandalia moja ya hoteli ambayo ni ndogo, haina hadhi ya kutumiwa na wachezaji wake mastaa kutoka nje ya nchi.“

 

Kwani mara baada ya kutua Zanzibar walipelekwa kwenye moja ya hoteli iliyoandaliwa na waandaaji wa michuano hiyo, lakini walipofika viongozi na wachezaji waliigomea na kuomba wabadilishiwe.“

Walivyogomea haraka waandaaji wakawapa hoteli nyingine yenye hadhi watakayoitumia kwa kipindi chote ambacho Yanga itakuwepo huko ikishiriki michuano hiyo,” alisema mtoa taarifa huyo.

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave a Comment