×

Dr. Dre Kulipa Bilioni 4 Za Matumizi Kwa Mkewe

GODFATHER wa Muziki wa Rap nchini Marekani ambaye ni mtayarishaji nguli wa muziki, Dr Dre amekubali kumlipa aliyekuwa mkewe Nicole Young dola milioni 2 (Sh bilioni 4.6) kwa ajili ya matumizi yake binafsi.

 

Nicole baada ya kufanikiwa kupewa talaka wiki kadhaa zilizopita alifungua kesi mahakamani akidai kupewa fedha za kujikimu, kesi ambayo ilimwendea vizuri na mahakama kuamuru Dr Dre amlipe mkwanja huo kabla ya Januari 11.

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye Jarida la The Blast, Jumatano hii, shauri la talaka la wawili hao lilisikilizwa tena na waliwakilishwa na wanasheria wao.

Makubaliano hayo yanasema Nicole atapokea kiasi hicho cha fedha kuanzia Jumatatu ijayo kwa ajili ya matumizi yake akiwa nyumbani kwake mjini Malibu, huku gharama nyingine ikiwemo ulinzi itakuwa juu yake.

Kwenye shauri hilo, Nicole ametoboa siri kwamba Dre anamiliki mtonyo mrefu wa dola milioni 250 (Sh bil 577.2) pia ana hisa kwenye Kampuni ya Apple.

Leave a Comment