
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, leo Januari 12, 2021 amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuboresha jezi za timu ya taifa , Taifa Stars, kwa kubandika jina la timu.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa Habari, Waziri alisema: “Ninawashukuru TFF kwa ushirikiano mkubwa na wizara katika kuhakikisha timu zetu za taifa zinafanya vizuri hasa kwenye mashindano ya CHAN ambayo tutaenda kushiriki hivi karibuni.

“Kwa upande wetu sisi kama wizara tunaahidi kuwa bega kwa bega na timu ya taifa na tutakuwa wote timu itakapoenda Cameroon, haya yote ni katika kuhakikisha tunaiunga mkono timu yetu.

“Pia ningeomba hizi jezi zetu za timu ya taifa ziboreshwe zaidi kwa kuandikwa jina la timu kwa mbele ili hata mtu wa nchi nyingine akiona hiyo jezi anatambua ni ya Tanzania.
