×

Mchungaji Jela Miaka 140 kwa Kubaka Binti Zake Wawili

MAHAKAMA nchini Kenya imemfunga kifungo cha miaka 140 jela mchungaji aliyewabaka wasichana wake wawili wa miaka 14 na miaka 16 na kuwapa mimba.

 

Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi wa Baricho, Anthony Mwicigi, alimhukumu Mchungaji John Gichira

kifungo cha miaka 70 kwa kila msichana. Mahakama iliamua kuwa hukumu hizo zitatekelezwa moja baada ya nyingine na hivyo mchungaji huyo ataishi jela miaka 140.

 

Mchungaji huyo kutoka kaunti ya Kirinyaga katikati mwa Kenya, mwenye umri wa miaka 51, alikiri kuwabaka watoto wake hivyo kuswekwa jela. Alimlaumu shetani kwa ubakaji huo  na akawaomba msamaha watoto wake na mahakama.

 

Hakimu mkazi, Anthony Mwicigi, alisema mchungaji huyo alipatikana na hatia kwa kukiri mwenyewe kuwabaka watoto wake na akaagiza hukumu dhidi yake itolewe tarehe 14 Januari, 2021.

 

Mchungaji huyo anayefahamika kwa jina la Gichina alikamatwa mahali alipokuwa amejificha baada ya polisi kuanzisha harakati za kumsaka.

 

Msichana mmoja tayari ana mtoto wa miezi saba na mwingine ana mtoto wa miezi mitano.

Leave a Comment