×

Mapokezi Ya Yanga Dar ni Balaa, Mashabiki Wafurika (Picha +Video)

 
KIKOSI cha Yanga wamewasili mchana wa leo Januari 15, 2021 kutokea Zanzibar na kupokelewa kwa shangwe na mamia ya mashabiki waliofika kwa wingi kuipokea timu hiyo huku jiji la Dar Es Salaam shughuli zikisimama kwa muda.
 
Msafara wa timu hiyo uliwasili bandarini mchana kisha wachezaji kuingia moja kwa moja kwenye basi la timu na kuelekea makao makuu ya klabu hiyo.
Msafara huo uliongozwa na kingo’ra kilichoongozwa na pikipiki ya Polisi huku pia kukiwa na gari nyingine moja ya polisi iliyobeba maaskari zaidi ya watano wenye silaha.

Leave a Comment