
TUME ya Uchaguzi (EC) imemtangaza Yoweri Museveni (76) aliyeongoza taifa hilo tangu mwaka 1986 kuwa Mshindi wa nafasi ya urais kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Januari 14, 2021.
Tume imesema Museveni amepata kura 5,851,037 sawa na asilimia 58.64 huku mgombea wa upinzani, Robert Kyagulanyi, (Bobi Wine) akipata kura 3,475,298 sawa na asilimia 34.83.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Simon Byabakama, amemtangaza Museveni kuwa rais mteule baada ya kufikisha 50%, ya kura.
Hapo awali ‘Bobi Wine’ aliyakataa matokeo hayo ya yaliyokuwa yanatangazwa na tume kwa madai kuwa kulikuwa na udanganyivu mkubwa wakati wa zoezi hilo la kupiga kura.
Rais Museveni ambaye aliingia madarakani mwaka 1986, ataendelea kusalia madarakani mpaka mwaka 2026, na anaingia kwenye orodha ya marais waliotawala kwa kipindi kirefu zaidi barani Afrika.