
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, chini ya Lebo ya Konde Gang Music Worldwide, Ibrahim Abdul ’Ibrah’ amesema kuwa anatamani kurudisha heshima kwa jamii.
Akizungumza na AMANI kwa njia ya simu Ibraah ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya karata tatu, amesema kati ya ndoto yake anazotamani kutimiza moja wapo ni kuweza kutoa misaada kwenye jamii hasa kwa watoto yatima na nyumba za ibada.
“Kutoa misaada hicho ni kitu kizuri sana, maana ukiwa unafanya hivyo wanakuombea dua na Mungu pia anapokea zile dua kwa haraka sana na unakuta unabarikiwa kwenye mambo yako kwenye vitu ambavyo nilikuwa naviwaza siku nikija kuwa na pesa moja wapo ni kutoa misaada,”alisema Ibraah.
NA KHADIJA BAKARI