×

DC Aingilia Kati Walinzi Kumpiga Aliyekuwa Akimuuguza Mama’ke

Sakata la Daudi Lefi aliyekuwa anamuuguza mama wake hospitali ya rufaa Mkoa wa Shinyanga kupigwa na walinzi wa Suma JKT wanaolinda hospitali hiyo limechukua mpya baada ya mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko kuingilia kati.

 

 

 

Leo Jumamosi Januari 23, 2021 Mboneko amefanya kikao na watuhumiwa, viongozi wa hospitali na aliyepigwa ili kubaini chanzo kabla ya kutoa maelekezo.

 

 

 

Tukio la kijana huyo kushambuliwa na walinzi hao lilitokea jana Ijumaa Januari 22, 2021 wakati akiwa wodi namba moja ya wanawake alikolazwa mama yake mzazi.

 

 

 

Alikuwa akichukua karatasi ya kwenda kuchukua dawa ndipo walinzi hao walipomtaka aondoke kwa madai kuwa muda wa kuona wagonjwa umekwisha na yeye kuwajibu kuwa anatafuta dawa za mgonjwa.

 

 

 

Leo Mboneko akiwa na kamati ya ulinzi na usalama amefika katika hospitali hiyo na kufanya kikao cha ndani na viongozi sambamba na watuhumiwa pamoja na kijana huyo.

 

 

 

Video za tukio hilo zilianza kusambaa jana zikimuonyesha kijana huyo akipigwa na walinzi hao na kuibua mjadala mitandaoni.

 

 

Wakati kijana huyo akishushiwa kipigo na walinzi hao, mdogo wake, Lidia Lefi alisikika akiwataka waache kumpiga ndugu yake kwa kuwa walikuwa wanakwenda kuchukua dawa.

 

 

Leave a Comment