×

Murray Aambukizwa Covid-19 Huenda Asiende Australia

ANDY MURRAY nyota wa mchezo wa tenis duniani (Mwingereza) amegundulika kuambukizwa ugonjwa wa Covid-19 kabla ya kusafiri kwenda Melbourne (Australia) kwenye michezo ya wazi.

 

Mchezaji huyo alionekana ameambukizwa Covid-19 na hivyo kumchanganya kwamba huenda asiende tena Australia katika michezo ya wazi (Australia Open).

 

Nyota huyo bingwa wa mchezo huo mara mbili wa mashindano ya Wembledon anasemekana ana dalili ndogo tu za ugonjwa huo.

 

Murray, anayeaminika kukumbwa na ugonjwa huo wakati wa majira ya machipuko bado ana matumaini kwamba ataruhusiwa kushiriki michezo hiyo mikubwa inayojulikana kama ‘Grand Slam’.

Leave a Comment