×

Mtv Mama…Modi, Harmo, Zuchu, Rostam Kimewaka Huko

KIMEWAKA huko! Ndivyo unavyoweza kusema kuelekea mwezi mmoja wa lala salama huko kwenye kinyang’anyiro cha tuzo kubwa za muziki wa Afrika almaarufu MTV Africa Music Awards (MAMAs) kwa mwaka 2020/21.

 

Umebaki takriban mwezi mmoja kufikia kilele cha tukio hilo ambapo presha inapanda na kushuka huku kila mmoja akitumia nafasi anayoipata kuomba kura kwa mashabiki wake.

 

Tukio hilo kubwa linatarajiwa kufanyika jijini Kampala nchini Uganda, Februari 21, mwaka huu kwa njia ya mtandao kutokana na mlipuko mpya wa janga la Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.

 

Nchi nyingi zimefunga mipaka yake kwa sasa.Wanamuziki wa Tanzania walioteuliwa kuwania tuzo hizo ni Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Rajabu Abdul ‘Harmonize’, Zuhura Othman ‘Zuchu’ na Kundi la ROSTAM linaloundwa na memba wawili wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma’ na Boniventure Kabogo ‘Stamina’.

Diamond au Mondi anatajwa kuwania vipengele viwili ambavyo ni Mwanamuziki Bora wa Mwaka Afrika na Alone Together Best Lockdown Performance (shoo aliyofanya mwaka jana wakati sehemu kubwa ya Dunia ikiwa karantini).

 

Kundi la ROSTAM linatajwa kwenye Kipengele cha Best Group (Kundi Bora la Muziki Afrika).Kwa upande wa Harmonize au Harmo anatajwa kwenye Kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Kiume Afrika huku Zuchu akitajwa kuwania Kipengele cha Breakthrough Act (Mwanamuziki Anayechipukia Afrika).

 

Wanamuziki wa Afrika wenye vipaji vikubwa waliochaguliwa kuwania tuzo hizi ni pamoja na Burna Boy, Busiswa, Davido, Mondi, Innoss’B, Kabza De Small, John Blaq, Master KG, Suspect 95, Sheebah, Soraia Ramos, Tiwa Savage, Yemi Alade na WizKid; wote hawa, kila mmoja ameteuliwa kuwania vipengele viwili.

Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter, Burna Boy anasema yeye ndiye Mwanamuziki Bora Afrika kwa sasa baada ya Fela Anikulapo Kuti; ubishi huo unatazamiwa kuamuliwa na tuzo hizo.

 

Wengine walioongoza kuteuliwa kuwania tuzo hizo kubwa barani Afrika ni Kundi la Muziki la cha Sao Tome na Principe –Calema; hawa wanawania vipengele vya tuzo tatu za Mwanamuziki wa Mwaka, Kundi Bora la Mwaka na Kundi Bora Linaloigiza Mtindo wa Muziki wa Kireno wa Lusophone.

 

LISTI KAMILI;Ifuatayo ni listi kamili ya wanamuziki walioteliwa kwa ajili ya Tuzo za MTV MAMA’s 2020/2021 na makundi yao walivyoshinda;

MWANAMUZIKI BORA WA KIKE; Simi (Nigeria) Sheebah (Uganda)Sho Madjozi (Afrika Kusini)Busiswa (Afrika Kusini)Yemi Alade (Nigeria) Soraia Ramos (Cape Verde)Tiwa Savage (Nigeria)

MWANAMUZIK BORA WA KIUME; Burna Boy (Nigeria)Innoss’B (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo)Kabza De Small (Afrika Kusini)Harmonize (Tanzania) Fire Boy DML (Nigeria)Master KG (Afrika Kusini)Rema (Nigeria)

 

KUNDI BORA LA MUZIKI; Blaq Diamond (Afrika Kusini)Sauti Sol (Kenya)Kabza De Small /DJ Maphorisa (Afrika Kusini)Calema (Sao Tome na Principe)Ethic (Kenya)ROSTAM (Tanzania)

 

MWANAMUZIKI BORA WA MWAKA; KWA JUMLA Burna Boy (Nigeria)Calema (Sao Tome na Principe)Diamond Platnumz (Tanzania)Master KG (Afrika Kusini)Davido (Nigeria) Tiwa Savage (Nigeria)Wizkid (Nigeria)

 

MWANAMUZIKI ALIYEPATA MAFANIKIO;Elaine (Afrika Kusini)T ems (Nigeria) Omah Lay (Nigeria)Zuchu (Tanzania)John Blaq (Uganda) Sha Sha (Zimbabwe) Focalistic (Afrika Kusini)

 

MWANAMUZIKI BORA WA HIP HOP;Nasty C (Afrika Kusini uspect 95 (Ivory Coast) Khaligraph Jones (Kenya)Kwesi Arthur (Ghana)NGA (Angola)OMG (Senegal)

MWANAMUZIKI BORA WA UGANDA; Sheebah Bebe CoolJohn Blaq Vinka Daddy AndreSpice Diana

MWANAMUZIKI BORA WA MUZIKI WA LUSOPHONE; Calema (Sao Tome and Principe) Preto Show (Angola) Anna Joyce (Angola) Mr Bow (Msumbiji) Nelson Freitas (Cape Verde) Soraia Ramos (Cape Verde)

 

MWANAMUZIKI BORA WA MUZIKI WA KIFARANSA;Innoss’B (Jamhuri ya idemokrasia ya Kongo) Suspect 95 (Ivory Coast)Dip Doundou Guiss (Senegal)Stanley Enow (Cameroon)Fally Ipupa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo)Gaz Mawete (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo)

MWANAMUZIKI BORA WAKATI WA LOCKDOWN;

Diamond Platnumz (Tanzania) -Africa Day Benefit Concert Black Motion (South Africa) -Red Bull RendezvousNiniola FT Busiswa (Nigeria/Afrika Kusini) -Africa Day Benefit Concert Singuila (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) -DCDR SeriesAKA (Afrika Kusini) -AKA TVYemi Alade (Nigeria) -Poverty (live session)

UMUHI WA TUZO ZA MTV MAMAs

Tuzo za MTV MAMAs zilianzishwa mwaka 2008, zilikuwa maalum kwa ajili ya wanamuziki wa Afrika na kila mwaka Taifa moja kutoka barani Afrika hupewa kibali cha kuwa mwenyeji.

 

Kwa Afrika Mashariki ni Kenya na Uganda waliowahi kupata kibali hicho, lakini ipo siku moja zitafanyika nchini Tanzania!Ili kuwapigia kura wanamuziki wa Kitanzania, tembelea Tovuti ya MTV MAMAs kwa kubonyeza link hii; https://www

Leave a Comment