
NEEMA imezidi kuwashukia wasomaji wa Gazeti la Spoti Xtra ambalo linazidi kutoa zawadi mbalimbali kupitia chemsha bongo inayoendeshwa ndani ya gazeti hili kwa kushirikiana na Kampuni ya Vunja Bei Mobile Shop ambao ni wauzaji wa vyombo vya majumbani.
Wiki hii washindi wawili, Juvenal Shayo mkazi wa Bunju na Patson Simon wa Vingunguti, walipatikana ambapo Patson alijishindia tea set, huku Juvenal akiondoka na seti ya glasi. Washindi hao wamekabidhiwa zawadi zao leo Jumatatu Januari 25, 2021.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi katika Ofisi za Gazeti la Spoti Xtra zilizopo Sinza Mori, Dar, Juvenal ambaye ni shabiki wa Yanga, alisema: “Mwanzoni nilikuwa siamini kama mshindi anapatikana kihalali, lakini baada ya kushinda zawadi hii nimeamini kuwa Spoti Xtra hakuna ujanjaujanja.
“Nawashauri pia Watanzania wenzangu wasikate tamaa, washiriki kwa wingi shindano hili, wanaweza kupata nafasi ya kujishindia zawadi kama nilivyoshinda mimi.
“Binafsi napenda kusoma Gazeti la Spoti Xtra kutokana na habari za uhakika ambazo zinaandikwa, pia napenda kusoma hadithi zilizopo ndani yake.
“Mimi ni baba wa familia, nina mke na watoto wawili, hivyo zawadi hii ya seti ya glasi itatusaidia kama familia. Nawashukuru sana Spoti Xtra kwa zawadi hii.”
Naye Patson ambaye ni shabiki wa Simba, alisema: “Mimi ni mdau mkubwa wa magazeti ya Spoti Xtra kutokana na ubora wake na aina ya habari zinazoandikwa ni za kweli hata ukipita kwenye vyanzo vingine unazikuta.

“Mwanzoni nilikuwa siamini kama mtu anaweza kushinda kweli, lakini baada ya kujishindia zawadi hii nimeamini kuwa washindi wote wanapatikana kihalali bila upendeleo wowote.
“Kwa upande wangu mimi ni shabiki wa Simba, kupitia Gazeti la Spoti Xtra huwa napata fursa ya kupata habari za timu yangu ambazo ukisoma magazeti mengine huzikuti.”
Mhariri wa Gazeti la Spoti Xtra, Omary Mdose, alisema: “Tunawashukuru washirika wetu Kampuni ya Vunja Bei Mobile Shop ambao ndiyo wadhamini wa chemsha bongo hii, nawaomba wasomaji wetu wazidi kusoma gazeti letu kwani ni gazeti pekee nchini ambalo limesheheni habari na takwimu zenye ubora tofauti na magazeti mengine.
“Pia wasiache kushiriki chemsha bongo kwani tunaelekea ukingoni, tunakuja na funga kazi ambapo tutatoa zawadi kubwa zaidi ya hizi.”

Naye mwakilishi wa Kampuni ya Vunja Bei Mobile Shop, Kissa Daniel, alisema: “Sisi kama Vunja Bei kwa kushirikiana na Spoti Xtra tumeendelea kutoa zawadi mbalimbali kwa wasomaji wetu ikiwemo friji, brenda, seti ya vyombo na vitu vingine vingi. Kikubwa wasomaji wazidi kusoma Gazeti la Spoti Xtra ili wawpate fursa ya kuibuka na zawadi kutoka Vunja Bei.”
Spoti Xtra kwa kushirikiana na Vunja Bei Mobile Shop, imeanzisha chemsha bongo hiyo ambayo lengo kubwa ni kuwaleta karibu wasomaji wake.
Kwa sasa Gazeti la Spoti Xtra linapatikana mtaani mara tatu kwa wiki, Alhamisi, Jumapili na Jumanne huku bei ikiwa ni ileile, Sh 500 tu. Ili ushiriki chemsha bongo hii, nunua Gazeti la Spoti Xtra, funua ukurasa wa pili utakutana na maelekezo yote.
PICHA ZOTE: MUSA MATEJA