The House of Social Media
gunners X

Baraza la Seneti Lapokea Mashtaka Dhidi ya Trump

0

BARAZA  la Wawakilishi la Bunge la Marekani limewasilisha hati ya mashtaka mbele ya Baraza la Seneti dhidi ya rais wa zamani Donald Trump na kufungua njia ya kuanza kwa shauri la pili la kihistoria.

Wawakilishi tisa walioteuliwa kuongoza mchakato huo wamewasilisha shtaka moja pekee linalomtuhumu Trump “kuchochea uasi” baada ya wafuasi wake kuvamia majengo ya Bunge mjini Washington mapema mwezi huu.

 

Wakitembea kwa mwendo wa polepole wawakilishi hao waliwasilisha hati ya mashtaka mbele ya Baraza la Seneti na kufungua njia ya kuanza kwa shauri la kihistoria kwa kiongozi wa taifa hilo kushtakiwa mara mbili na Bunge.

 

Mwakilishi wa jimbo la Maryland Jamie Raskin ndiye alisoma shakta dhidi ya Trump ndani ya ukumbi wa Baraza la Seneti, ambako rais huyo mstaafu bado uungwaji mkono kutoka maseneta wa chama chake cha Republican.

Kuwasilishwa kwa hati hiyo ya mashtaka iliyoidhinishwa na Baraza la Wawakilishi linaloongozwa na chama cha Democrat mnamo Januari 13 kunafungua njia ya kuanza kwa shauri dhidi ya Trump katika wiki ya pili ya mwezi Februari.

 

Kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti Chuck Schumer amesema wajumbe 100 wa baraza hilo ambalo watafanya kazi kama mahakimu wataapishwa leo Jumanne na tayari wito wa kufika mbele ya baraza umetumwa kwa Bw. Trump.

 

Wanasiasa wa Democratic na Republican walikubaliana kuchelewesha kwa muda wa wiki mbili kuanza kwa shauri hilo ili kumruhusu Trump kuandaa utetezi wake dhidi ya shtaka linalomkabili la “kuchochea uasi” na kuruhusu Baraza la Seneti kuidhinisha wateule wa nafasi mbalimbali za utawala rais Joe Biden.

 

Mara hii kesi hiyo itaongozwa na makamu mwenyekiti wa Baraza la Seneti Patrick Leahy kutoka chama cha Democratic ambaye ni seneta mkongwe zaidi badala ya jaji mkuu wa Marekani John Roberts aliyeongoza shauri la kwanza dhidi ya Trump wakati alipokuwa rais.

 

Spika wa Baraza la Wawakilishi akionesha hati ya mashtaka aliyoitia saini kabla ya kuwasilishwa kwa Seneti.

Makamu mwenyekiti wa Baraza la Seneti kwa kawaida ndiye huongoza mashtaka dhidi ya kiongozi yeyote asiye rais wa Marekani ambaye shauri lake limewasilishwa mbele ya chombo hicho.

 

Wakati hayo yakijiri, rais Joe Biden ameonesha kutojishughulisha kabisa na kile kinachoendelea Bungeni dhidi ya mtangulizi wake na shauri linalomkabili.

 

Wanasiasa wa chama cha Biden wameendelea kutoa wito wa Trump kuwajibishwa kwa kile wanasema alichochea uasi dhidi ya utawala wa Marekani.

 

Mwakilishi wa chama cha Democratic Jerry Nadler ambaye pia ni mwenyeketi wa kamati ya mahakama yaBaraza la Wawakilishi amesema sasa ni wajibu kwa Baraza la Seneti kufanya kazi yake kwa kumtia hatiani Trump na kumzuia kutowania tena wadhifa utakaomwezesha kusababisha madhara kwa taifa hilo.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply