
MEYA wa manispaa ya Moshi, Juma Raibu Juma, amewataka wajumbe waliovaa barakoa katika kikao cha baraza la madiwani kuzivua kwa madai kuwa manispaa hiyo ipo salama.
Ametoa agizo hilo leo Alhamisi, Januari 28, 2021, wakati wa ufunguzi wa kikao cha bajeti cha baraza hilo alipowataka madiwani waliovaa barakoa kusimama na kisha kuwataka wazivue.