×

Wanawake Arusha Waandamana Kisa Mauaji ya Mwenzao

JESHI la Polisi mkoani Arusha jana jioni lilitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanawake waliokuwa wakiandamana na kufunga barabara wakizuia kuzikwa kwa Anna Ng’ida aliyeuawa kwa kunyongwa na kutupwa katika korongo.

 

 

Tukio hilo lilitokea jana jioni katika Kata ya Mateves ambayo ipo nje kidogo ya jiji la Arusha. Wakizungumza katika maandamano hayo, wanawake hao walikuwa wanataka uchunguzi wa kina ufanyike kuhusiana na vifo vya wanawake tisa vilivyotokea hivi karibuni katika eneo hilo.

 

 

Salina Haruni alisema wameshangazwa na kitendo cha kushambuliwa kwa mabomu wakati wao walikuwa wanataka uchunguzi wa vifo hivyo kufanyika. “Huyuni mtu wa tisa kuuawa, hatuoni jitihada za kukamatwa watuhumiwa,” alilalamika mwanamke huyo.

 

 

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha , Salum Hamduni,  alieleza kwamba polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi ili  kuwatawanya watu hao

 

Alisema kabla ya nguvu kutumika waliwataka watu hao kutawanyika lakini waligoma. Hata hivyo, aliomba radhi kwa tukio hilo na kuahidi uchunguzi utafanyika ili kuwakamata watuhumiwa. Baada ya majadiliano baina ya pande zote hatimaye mwili wa mwanamke aliyeuawa ulizikwa.

Leave a Comment