×

Liundi: Mama Alitunywesha Sumu, Wadogo Zangu Wakafariki

Mtangazaji nguli nchini, Taji Liundi, amefunguka kuhusu maisha yake binafsi na mchango wake katika tasnia ya muziki. Taji aka Master T ambaye amefanya kazi na vituo mbalimbali vya redio ikiwemo Radio One na Times FM tangu miaka ya 1980 amefunguka mengi wakati akihojiwa na kipindi cha Salama Jabir.

 

 

Taji amesimulia kisa cha kusisimua na kusikitisha ambapo mama yake mzazi aliamua kuwanywesha sumu yeye na wadogo zake watatu, tukio lililosababisha wadogo zake watatu kufariki dunia huku yeye akiponea chupuchupu.

 

 

Tukio Hilo lilitokana na mgogoro wa ndoa baina ya mama yao na baba yao kutokana na kukosekana kwa uaminifu hasa upande wa mzee wake, baada ya mama Taji,  Agnes Doris Liundi,  kugundua hilo aliazimia kujiua yeye na wanaye na ndiyo kisa cha kuwanywesha sumu wanaye.

 

 

Mama Taji alihukumiwa kunyongwa mpaka kufa na Mahakama kabla ya kupewa msamaha wa Rais na hayati Baba wa Taifa J. K. Nyerere. Baba yake Taji  alikuwa mwanasheria, Jaji wa Mahakama Kuu na hatimaye Msajili wa Vyama vya Siasa mwaka 1992.

 

 

Pia Taji ameeleza alivyoanza kutangaza Radio One, kipindi chake alichokianzisha cha DJ Show na kuwa mtangazaji wa kwanza kucheza Bongo Fleva kwenye redio, kabla ya kuwaachia mikoba kina Mike Mhagama baada ya kuondoka katika kituo hicho.

 

Leave a Comment