
MSANII wa muziki kutoka lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Februari 1, 2021, ameachia rasmi albam yake ya kwanza iitwayo ‘Sound from Africa’ ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki zake.
‘Sound From Africa’ imekamilishwa na nyimbo 23 zilizowakutanisha wasanii wengi wa kimataifa ambao wengine tayari aliwahi kushirikiana nao mwanzo na wengine ikiwa ni mara ya kwanza kushirikiana nao.
Hii ni moja kati ya albam kubwa Afrika kutokana na wasanii aliowashirikisha humo ndani ambapo katika albam hiyo amekutana na wasanii wengi.