
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imemfikisha mahakamani aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu katika Chama cha Wafanyakakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kwa makosa ya 48 yakiwemo ya utakatishaji wa feha zaidi ya Tsh milioni 410.
Akimsomea hati ya mashtaka Mwendesha mashtaka kutoka Takukuru, Lupyana Mwakatobe amesema kuwa mshtakiwa Sospeter Galus Omollo katika terehe tofauti kati ya Septemba 22, 2016/17 katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salam anadaiwa kughushi hundi mbalimbali akijua kufanya hivo ni kosa kisheria.

Imeelezwa kuwa Mshtakiwa Omollo akiwa katika Tawi la Benki ya BOA iliyopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam akiwa na nia ovu alighushi hundi mbalimbali ambazo zilionesha zimesainiwa na Kibwana Ramadhani lengo likiwa ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo Hakimu Mkazi Kisutu Yusto Ruboro amesema kuwa makosa yanayomkabili mshtakiwa hayana dhanamana kwakuwa yapo ya utakatishaji fesha na uhujumu uchumi hivyo mshtakiwa amepelekwa segerea hadi itakapotajwa tena Februali 16, 2020.
Makosa mengine yanayomkabili ni pamoja na kughushi nyaraka kinyume na kifungu cha335(a)(d)(1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura 16 rejeo ya mwaka 2019 ambapo mshatakiwa anadaiwa kutakatisha fedha kiasi cha Tsh. 410,170,000.