×

Gomez Amuita Mkude Kikosini Fasta

KATIKA kuhakikisha kikosi chake kinaendelea kuwa imara na cha ushindani zaidi, Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes amemuita kiungo wa timu hiyo, Jonas Mkude ili kuweza kuona uwezo wake na kumtumia katika mechi za Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Mkude aliitwa jana na kutakiwa kuanza mazoezi na kikosi cha Simba baada ya kukaa mbali na kikosi hicho kwa muda mrefu tangu mwishoni mwa mwaka jana kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu.

 

Aidha Mkude ambaye amekuwa akitegemewa sana katika eneo la kiungo mkabaji kutokana na uwezo wake, aliomba radhi uongozi wake na mashabiki wa timu hiyo wiki iliyopita kwa kile alichokifanya kwa kutaka asamehewe ambapo alikuwa akisubiria ruhusa kutoka kwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mkude amesema kuwa, uongozi wa timu hiyo ulimuita jana na kumtaka aanze mazoezi na wenzake haraka na hadi mchana tayari alishajiunga na wenzake.

 

“Uongozi umenipigia simu niweze kwenda kujiunga na timu katika mazoezi yanayoanza leo (jana), kuhusu suala la wachezaji wenzangu kutaka kuzungumza na mimi sijui kitu chochote na wala sijui kama kuna jambo kama hilo ninachofahamu ni kwamba niliambiwa nifike kambini haraka na nimetii hilo,” alisema Mkude.

 

Simba kesho itajitupa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kupambana na Dodoma Jiji, kabla ya Jumapili ijayo kuvaana na Azam FC kwenye Uwanja wa Mkapa.

STORI: KHADIJA MNGWAI, Dar es Salaam

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment