
PAZIA ni moja kati ya Tamthilia pendwa kabisa kwa sasa inayoruka kupitia Maisha Magic Bongo ndani ya Dstv.
Imesheheni visa vya kusisimua kuhusu maisha ya mahusiano ya vijana.
Karibu tuendelee kuisoma hapa:
Katika wiki iliopita kwenye episode ya 9 hadi 12 kuna yale tuliyoyaona yakiendelea kwenye PAZIA moja; ni jinsi msimamo wa hawa vijana wakionesha msimamo wao wa mapenzi.
Tuliweza kuona jinsi kijana Edu akiingia katika mtego baada ya jumba bovu kumuangukia baada ya kusadikika kuwa amembaka Regina huku Regina akitumia kama fimbo ya kutaka aolewe naye wakati anampenda kwa muda mrefu lakini cha ajabu Edu anampenda Groly na Glory naye mapenzi yake yako kwa Jemo huku Jemo naye akimpenda Regina.

Hospitali tuliona Dr Love akipewa likizo ya miezi 6 baada ya kugundulika mchezo wake mchafu wa kumtorosha Regina, pia tuliona Regina akiwaambia wazazi wake msimamo wake wa ndoa na kuwaambia ana mimba ya Edu huku mama Regina akionekana kumsapoti Regina katika suala lake la ndoa.
Changamoto kubwa ikawa ni kwa baba yake Regina ambaye alionekana kuchukizwa na suala hilo akitaka mwanaye aende chuo, nje ya nchi. Regina anaondoka zake kwa hasiria nyumbani, akimuacha baba na mama yake mezani.
Edu naye tulimwona akienda kwa mama yake Groly kumuambia ukweli kuwa hahusiki na yanayoendelea juu yake kwani hajambaka Regina kama wanavyomshutumu ila ni mchezo uliopangwa na Groly na yeye anampenda Regina.
Mipango ya harusi ikiwa imepamba moto, mama Regina anaahidi kulipa shilingi milioni 20 kugharamia harusi ya binti yake huyo kipenzi huku baba Regina akisusia ndoa kwa msimamo wa kutaka binti yake aende kusoma nje ya nchi.
Fred anaamua kueleza ukweli kuwa siku ya club, Regina alibaki na Edu hivyo tunaweza kuona Edu anajitetea bure ila yeye ndio mhusika wa kwanza.

Mwishoni tuliweza kumaliza kwa mama yake Regina anampelekea mualiko mama Groly akimtaka Glory awe msimamizi wa Regina huku Glory naye akitaka Jemo awe msimamizi wa Edu. Wakati huo, tunaona Jemo ametangaza vita kwa Edu kwa kuwa yeye ndio alitakiwa kumuoa Regina.
Usikose episode ya 13 hadi 15 ambapo tutaweza kuona mipango ya harusi ya Regina ikiwa imekamilika lakini kanisani Edu hakuweza kutokea huku Jemo akituma majambazi wamuue Edu hivyo harusi ikiwa inaendelea kanisani Jemo anaomba yeye amuoe Regina na kusema Edu amefariki.

Kupata mwendelezo wa uhondo huu kupitia channel ya Maisha Magic Bongo kuanzia Jumatatu hadi Jumatano kuanzia saa moja na nusu usiku, usikose!
View this post on Instagram