
KUMEKUWA na maoni mengi kuhusu mtazamo wa Max Rioba baada ya video yake kusambaa mitandaoni akisema wanawake wanatakiwa wajitume na si kutegemea pesa za kupewa na mpenzi/mume (kuhongwa) ili kuendesha maisha yao.
Hata hivyo, wanawake/wasichana wengi wameonekana kupokea kwa mtazamo hasi kauli hiyo na kumshushia matusi ya kutosha.
Global TV Online imefanya exclusive intererview (mahojiano maalumu) na Max Rioba ili kujua ni nini hasa alimaaanisha na alikuwa na lengo gani kutoa kauli kama hivyo kwa wanawake.