
Mkuu wa mkoa Mbeya, Albert Chalamila amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo kuwasafirisha bure wananchi wote wa kijiji cha Ifumbo wanaougua ugonjwa usiojulikana kwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya ili wachukuliwe vipimo na hatimaye waweze kuutambua na kuwapatia tiba.
Kauli hiyo ya Bw.Chalamila ameitoa Siku moja baada ya kuripotiwa uwepo wa ugonjwa usiojulikana katika kata ya Ifumbo wilayani Chunya baada ya kupata maelezo ya wananchi kuhusu uwepo wa ugonjwa huo usiofahamika kijijini hapo.