×

Ndayiragije Adaiwa Kuvunjiwa Mkataba Stars

TETESI za kuvunjwa kwa mkataba wa kocha wa timu ya taifa la Tanzania ‘Taifa Stars’, Etienne Ndayiragije na Shirikisho la soka nchini (TFF) zilizosambaa kwenye mitandao wa Kijamii zimezua taharuki kwa wadau mbalimbali.Inaelezwa, kwa mujibu wa ukurasa wa Mtangazaji maarufu wa michezo nchini, Maulid Kitenge kuwa tayari yamefanyika makubaliano ya kusitishwa kwa mkataba wa Ndayiragije baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

 

Ujumbe wa Kitenge ulisomeka kuwa, “TFF na Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Taifa Stars Ettiene Ndayiragije wakubaliana bora yaishe, wavunja Mkataba.”

 

Hata hivyo TFF, kupitia kwa katibu mkuu wake, Wilfred Kidao haijakanusha wala kukubali taarifa hizo ikidai ina utaratibu wa kujulisha umma juu ya masuala kama hayo.

 

“Unajua kila taasisi mahali popote pale lazima iwe na utaratibu wake wa kutoa taarifa kwa hiyo ni vema kuheshima taratibu hizo,” alisema Kidau na kukatisha mawasiliano.

 

Tetesi za kuvunjwa kwa mkataba wa Ndayiragije zimevuma mitandaoni ikiwa ni siku chache tangu kikosi cha Taifa Stars kirejee nchini kikitokea Cameroon ambako kilikuwa kikishiriki fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezanji wa ndani (Chan).

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment