
STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba, amethibitisha kuwa akaunti yake ya YouTube ya Alikiba sasa ipo mikononi mwake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Alikiba amewaambia mshabiki wake wawe tayari na wa-subscribe akaunti hiyo kwa ajili ya kupokea muziki wake.
Ikumbukwe Alikiba baada ya kuachana na aliyekuwa meneja wake wa zamani, Seven Mosha, ilielezwa kuwa akaunti hiyo ipo chini ya Seven na takribani mwaka sasa hakuwa anaitumia kwa ajili ya kuweka ngoma zake na badala yake alikuwa akitumia akaunti ya Kings Music ambayo pia ipo chini yake ila nyimbo zinazoweka katika akaunti hiyo ni pamoja na za wasanii wa lebo hiyo.
Akaunti hiyo tayari ina subscribers zaidi ya laki saba na tayari ameanza kuweka maudhui.
