×

Zari Ampa Jina Jipya Mwanaume Wake Siku ya Wapendanao

HISTORIA inaonesha kwamba, msimu wa Siku ya Wapendanao (Valentin’es Day), mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, huwa hakosi jambo lake na ndivyo ilivyotokea msimu huu.

 

Wakati siku hiyo ikifurahiwa na wapendanao jana, Zari na mwanaume wake mpya ndiyo kapo nyingine iliyozungumzwa zaidi na kuteka kurasa za udaku.

 

Zari, kama alivyotumia msimu huu kuachana na mzazi mwenza, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, aliyezaa naye watoto wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan, msimu ule wa mwaka 2018, ndivyo alivyoutumia ukurasa wake wa Instagram jana kumtangaza mwanaume wake mpya.

 

Kama hiyo haitoshi, ndiyo msimu pia alioutumia mwaka 2019 kumtangaza mpenzi wake mwingine mpya aliyeitwa Cedric Fourie alimaarufu King Bae kabla ya kuachana mwaka jana.

 

Ndivyo ilivyokuwa pia enzi za aliyekuwa mumewe, marehemu Ivan Ssemwanga kwamba lazima msimu kama huo afanye tukio ambapo miaka ile aliyokuwa na jamaa huyo, alikuwa akipewa zawadi mbalimbali yakiwemo magari ya kifahari kama Lamborghini, Bentley, Ferrari, Maserati na mengine ya bei mbaya.

 

“Happy Valentine’s Day my 8.6 lovers,” aliandika Zari jana wakati akimuanika mwanaume wake huyo.

Ujumbe ulikuwa ni hitimisho ya ujumbe mbalimbali ambazo Zari amekuwa akiweka kwenye ukurasa wake kama;“Usiniumize moyo wangu mdogo…mwanaume wangu, muite Farasi Mweuzi!”Zari amekuwa akimtambulisha mwanaume huyo kwa jina la Farasi Mweusi kutokana na weusi wake.

 

Zari anasema moyo unataka kile unachokitaka hivyo amejikuta kwenye mahaba mazito kwa mara nyingine katika msimu huu wa Valentine.

 

“Watu wengi wanatamani kumuona kwenye makundi yao ya WhatsApp, naomba msiniweke kwenye kundi la watu wa aina hiyo.

 

Nimekataa kuwa mmoja wao…furaha inaishi hapa, kama yataisha kwa machozi, acha iwe hivyo, kwani wewe (watu wanaomuonya ataachwa tu) unapoteza nini kwenye maisha yako?”

 

Anahoji Zari na kuomba aachwe kama ni jahazi kuzama, acha lizame.Zari alitengana na Diamond au Mondi Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) ya mwaka 2018 kabla ya kuangukia kwa King Bae na sasa yupo mikononi mwa Farasi Mweusi

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

Leave a Comment