
MWILI waaliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mpindunzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hammad, leo Februari 18, 2021, unatarajiwa kufanyiwa swala katika msikiti wa Maamuri Jijini Dar es salaam kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa ajili ya mazishi.
Baada ya swala hiyo, mwili wa Maalim Seif umewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Pemba, Zanzibar kwa maziko yanayotarajiwa kufanyika baadaye leo, Februari 18.
Maalim Seif alifariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa.