×

Magufuli: Nimewahi Kuwa Dereva Teksi – Video

 

Rais John Magufuli amesema kazi anayofanya ina changamoto zake kwa kuwa anatamani kuendesha gari lakini anazuiwa na ametoboa siri kuwa alikuwa dereva teksi wakati akisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

 

 

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Jumatano Februari 24, 2021 wakati akizindua daraja la juu la Ubungo. “Nimefurahi, kazi hizi saa nyingine ni mateso wakati nasoma Chuo Kikuu pale nilikuwa napaki teksi bubu pale, napakia pale lakini leo hata nikiomba niendeshe hata kidogo nazuiliwa lakini ndiyo maisha.

 

 

“Kwa hiyo maisha ya Ubungo mimi nayajua, unajua kuna mtu anafikiri mimi sijui! Naijua sana, najua Profesa Kitila Mkumbo unaijua sana Ubungo umekaa miaka 18 lakini na mimi nimekaa hapa miaka mingi kidogo inawezekana saba, nane au tisa hivi kwa hiyo ninapoona mabadiliko haya nawapongeza sana Dar es Salaam,” amesema.

 

 

Amesema wakati eneo hilo mpaka Kimara nyumba za wananchi zikivunjwa kukwepa ujenzi wa barabara, majengo ya Serikali hayakubomolewa suala ambalo hakulipokea vizuri.

 

 

“Hatuwezi tukaongoza katika kuvunja sheria, sheria ni msumeno walisema kipande cha Tanesco kipo ndani ya barabara namkumbuka mtani wangu mzee Pinda akiwa Waziri Mkuu wakati huo akisema mtu kweli anaweza kwenda kuvunja jengo lile?  Sasa mwambieni tumelivunja, mtashangaa kwamba anamsema aliyekuwa Waziri Mkuu wake! Ndiyo sheria ni msumeno.”

Leave a Comment