×

Shigongo Aingia Darasani Kufundisha Biology Fomu 4 & 6 – Video

 

MBUNGE wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, ameamua kuingia darasani na kufundisha somo la Biology kwa wanafunzi wa kidato cha nne na  cha sita katika Shule ya Sekondari Nyehunge iliyopo Halmashauri ya Buchosa.

Mhe. Shigongo akiwa darasani katika kidato cha nne amefundisha mada ya Mfumo wa Mzunguko wa Damu katika mwili wa binadamu (Circulatory System).

Amewaeleza wanafunzi hao kuwa ili damu iweze kusambaa katika mwili wa binadamu inatakiwa kusukumwa na moyo ambayo ndiyo injini ya kuendesha mwili wa binadamu, akiongeza kwamba moyo unaundwa na mishipa mbalimbali inayofanya damu isambae vizuri katika mwili wa binadamu.

 

Kwa wanafunzi wa kidato cha sita, Mhe. Shigongo amefundisha mfumo wa kukusanya taka mwilini (Excretion System) amewaeleza wanafunzi kuwa mfumo huo utatumika kuulinda mwili, kukusanya take mwili pamoja na kuweka sawa maji katika mwili.

 

Amewaeleza kuwa mfumo huo unamsaidia mtu kutoa maji yake mwilini (mkojo) na sumu (toxins) hivyo kufanya mwili uwe katika hali ya kawaida huku akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao kitaifa, jambo ambalo litawasaidia kutimiza ndoto zao.

 

Aidha,  amewaahidi kwa wanafunzi wambao watafanya vizuri kidato na nne na sita kutoka shule ya Sekondari Nyehunge pamoja na shule zingine za jimbo hilo watapata zawadi kutoka katika ofisi yake.

 

Awali kabla ya kuingia darasani na kufundisha,  alipata nafasi ya kuzungumza na walimu wa shule hiyo na kuwaeleza kuwa nia yake ni kuona Shule ya Sekondari Nyehunge inaongoza kiwilaya, mkoa na taifa kwani uwezo wanao na kuwaomba wafundishe kwa bidii kila mwalimu aonyeshe dhamira ya kuinua kiwango cha ufaulu katika somo lake  ili kufikia malengo ya kuondoa zero kidato cha nne na sita na kuongeza ufaulu katika Jimbo la Buchosa.

 

Amesema katika uongozi wake anataka ufaulu uongezeke kwa kasi kubwa kwani watoto wana uwezo mkubwa wa kufanya vizuri kama kila mmoja atatimiza majukumu yake katika kumsaidia mwanafunzi.

 

Leave a Comment