
NYOTA maarufu wa mchezo wa gofu, Tiger Woods, amefanyiwa upasuaji wa mguu wake wa kulia baada ya kupata ajali mbaya ya gari.
Tiger alipata ajali hiyo juzi katika Mji wa Los Angeles, Marekani, baada ya gari lake kupoteza mwelekeo ambapo aliumia katika maeneo tofauti ya mwili wake.

Katika ajali hiyo, gari ilionekana ikiwa imeharibika vibaya na kulazimika Tiger kutolewa kwa vifaa maalum na kukimbizwa hospitali kwa matibabu ya haraka.
Taarifa iliyotolewa ilisema: “Tiger ameamka baada ya upasuaji wa mguu wake wa kulia na anaendelea vizuri kwa sasa.“Tunashukuru kwa sapoti ya kila kitu kwa kipindi kigumu kama hiki ambacho anapitia Tigerna anaendelea vizuri, kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa madaktari.”