
KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amefunguka kwa kumsifia kiungo mwenzake raia wa Angola, Carlos Carlinhos kuwa ni mchezaji anayeweza kuisaidia timu wakati mgumu.
Carlinhos amefunga mabao matatu ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu kati ya mabao 34 yaliyofungwa na Yanga msimu huu na kutoa asisti mbili.
Fei Toto amesema kuwa, Carlinhos ni mchezaji mwenye uwezo wa kubadilisha mchezo na kuisaidia timu wakati mgumu.
“Carlinhos ni mchezaji mzuri, ana maamuzi ya haraka na anatoa ushirikiano kwa wenzake, ana uwezo wa kubadili mchezo na matokeo,” alisema Fei Toto.
Kwa sasa Yanga ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na alama 49 wakifuatiwa na Simba wenye alama 42