
RAIS wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, amekutwa na hatia katika kesi ya ufisadi iliyokuwa inamkabili. Rais huyo aliongoza kuanzia 2007-2012.
Sarkozy (66) amekutwa na hatia ya kujaribu kumhonga Jaji kwa kumpa nafasi ya juu ya kazi huko Monaco ili ampatie taarifa kuhusu uchunguzi wa jinai katika chama chake cha siasa.
Akitoa hukumu hiyo, Jaji amesema rais huyo wa zamani anaweza kutumikia kifungo cha ndani na inatarajiwa Sarkozy atakata rufaa.