×

Mwanza: Vikoba Kufungwa Aprili 30

MKURUGENZI wa Usimamizi wa Mabenki wa Benki Kuu, Jerry Masyenene amesema ifikapo Aprili 30, mwaka huu vikoba abavyo havijasajiliwa havitatambulika katika sekta ya fedha.

 

 

Hayo yemebainishwa katika ufunguzi wa mafunzo ya miongozo na mfumo wa usajili wa vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha uliofanyika mkoani Mwanza kwenye ukumbi wa banki kuu uliyokutanisha Maafisa Tehama na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Mkoani Mwanza’ Kigoma na Shinyanga.

 

Masyenene amesema faida za kujisajili ni kupunguza wimbi la umasikini katika jamii, kutengeneza mamilioni na kupata mikopo kwa haraka kutokana na kutambulika katika sekta za kifedha.

 

 

Alisema kila kikundi kinapaswa kuwa na wanachama 10 -50 kwani kikiwa zaidi na pungufu hakitaandikishwa na hakuna gharama yoyote kila chama kitatakiwa kuwa na katiba ambayo imepitishwa kwenye mkutano mkuu mmoja na kutakuwa na mkaguzi wa kikundi na ukaguzi kutoka Tamisemi.

 

 

“Na baada ya usajili watapewa cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa halmashauri kupitia vikundi hivyo tutapata mabilione yaan kuchachua uchumi kuliko kuwa wanazifungua ndani na kuzuia kuzurumiana.

 

 

Alisema huko nyuma kulikuwa na makampuni mengi yanayotoa mikopo lakini hakukuwa na usimamizi wowote hivi sasa kampuni zote zinazotoa mikopo zipo chini ya usimamizi wa benki kuu kwani imetengeneze nyaraka zote muhimu zitakazosimia vikundi hivyo.

 

Vikundi vitaingizwa kwenye mkata ya mkopo ili kuzuia mtu kukopa tena katika taasisi wala benk yeyote na uhusiano wako na pesa utakuwa umeisha na kwa sasa tumejidhatiti katika data kwa kutumia taarifa zako kwa kutumia namba za NIDA za mtu husika.

 

 

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Emmanuel Kipole amewata maafisa maendeleo kuwashirikisha elimu waliyoipata watendaji wa kata, mtaa navijiji kwa vikundi hivyo huanzia huko.

 

Na Leah Marco, Mwanza

Leave a Comment