×

RC Kunenge Achukizwa na Viongozi Wanaochelewa Kwenye Vikao

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Aboubakar Kunenge akizungumza leo katika kikao Cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewataka wajumbe wa Bodi ya Barabara kuhakikisha vipaombele vya Ujenzi wa Barabara vinazingatia mahitaji ya wananchi.

 

RC Kunenge amesema hayo wakati wa kikao Cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kumekuwa na ujenzi wa Barabara ambazo sio kipaumbele cha wananchi na kuacha zile zenye uhitaji zikibaki kuwa mbovu jambo linalosababisha kero kwa watumiaji.

Kutokana na hilo RC Kunenge amesema kuanzia sasa ikitokea vikao vimepitisha mambo yasiyozingatia mahitaji ya wananchi walio wengi yakifika mezani kwake hatoyaidhinisha kwakuwa ameamua kuwa sauti ya waliowengi.

Katika hatua nyingine RC Kunenge ameonyesha kuchukizwa na tabia ya baadhi ya viongozi wanaochelewa kuhudhuria kwenye vikao na kusababisha vikao kuchelewa kuanza kitendo alichokiita utovu wa nidhamu.

Leave a Comment