×

Careen: Mwanamme Kumpa Pesa Mwanamke Si Kuhonga

 

BABY mama wa msanii Barakah The Prince ambaye ni Video Vixen, Careen Simba, amesema ni jukumu la mwanamme kumpa pesa mpenzi wake na anavyompa si kama anamhonga bali ni kumlinda na kumhudumia.

“Mwanamme kumpa pesa mwanamke ni jukumu lake, kwa kweli na kama mwanamke wako lazima umhudumie ingawa na yeye anatakiwa afanye kazi, siyo kila kitu mpaka amwambie mwanamme wake, ni jukumu la mwanamme kutoa pesa kwa mwanamke si kama unamhonga bali ni kumjali ili asije akaangaliwa na watu wengine mwisho wake akusaliti” ameeleza Careen Simba

Kwa sasa mrembo huyo anaigiza filamu na ametokea kwenye video ya wimbo mpya wa Kala Jeremiah.

Leave a Comment