
MEGHAN Markle na Prince Harry katika interview mpya na Oprah Winfrey wamesema hata kabla mtoto wao hajazaliwa baadhi ya wanafamilia ya kifalme nchini Uingereza walikuwa wakijadili rangi ya ngozi ya mtoto wao itakavyokuwa kama atakuwa mweusi kwani Meghan mama yake mzazi ana asili ya Afrika.
Kitendo hicho Meghan amekichukulia Kama ubaguzi wa rangi na kuongeza kuwa ilifika wakati akatamani kujiua kutokana na maneno hayo kwani wanafamilia hao walikuwa wakidai kuwa mtoto huyo akizaliwa hatakuwa na hadhi ya kuitwa Mwanamfalme kutokana na rangi yake.

Prince Harry amekiri hilo pia ingawa amesisitiza kuwa babu na bibi yake hawakuwa sehemu ya watu waliokuwa wakijadili rangi ya mtoto itakavyokuwa hata kabla hajazaliwa ingawa wanafamilia wengine ya kifalme walikuwa wakijadili hilo na yeye hakulipenda Hilo.
Kwa upande mwingine, Meghan na Prince Harry wamesema, baada ya familia ya kifalme kuwaondolea ulinzi binafsi, walikuwa nchini Canada na lilikuwa suala la ghafla ambalo hawakulitegemea lakini wanamshukuru sana Tyler Perry star wa Hollywood kwa kuwasaidia ulinzi binafsi na kutoa moja ya mijengo yake ya kifahari uliopo Carlifonia ambapo Meghan na Prince Harry walikaa kwa miezi mitatu.

Interview ya Oprah na wawili hao wakifunguka imetrend hasa kwakuwa Meghan na Prince Harry walishakiri kuwa vyombo vya habari vya Uingereza vilikuwa vimejaa ubaguzi wa rangi kwa jinsi vilivyokuwa vikimuundia zengwe mkewe kila uchao sababu tu ana asili ya afrika bila kusahau chokochoko za ubaguzi wa rangi ndani ya familia ya kifalme.
Kwa ujumla Prince Harry kwa muda mrefu Sasa amesimama imara na mkewe na sio kuwa upande wa familia ya kifalme anayotokea.