
KOCHA Pep Guardiola amekiri kuwa Manchester City kitendo cha kupigwa mabao 2-0 na majirani zao, Manchester United kimewapa somo.
Bruno Fernandes aliunga bao la kwanza kwa penalti kisha Luke Shaw akafunga bao la pili katika mchezo huo wa Premier League.Guardiola amesema: “Kuna muda hutakiwi kushinda mchezo ili ujifunze. Najua tut-akuwa habari kwa kuwa tumepoteza lakini habari kubwa ni kushinda mechi 21 mfululizo.
Matokeo haya yatatufundisha na kutuonyesha jinsi gani msimu ulivyo mgumu.“Ni somo, katika soka lolote linaweza kutokea, nawapongeza United.
”Kabla ya mchezo huo, mara ya mwisho kwa City kupoteza mechi katika ligi hiyo ilikuwa Novemba 21 dhidi ya Spurs.
Pamoja na kupoteza mchezo huo, Man City imeendelea kubaki kileleni kwa kuwa na tofauti ya pointi 11 dhidi ya maajirani zao hao wanaoshika nafasi ya pili.
Guardiola aliongeza: “Tunahitaji kushinda mechi sita au saba kati ya 10 zinazo kwa kuwa bado kuna pointi 30 za kuwania ubingwa.”