×

Mserbia Kumrithi Kaze Yanga

KOCHA wa zamani wa Township Rollers ya Botswana, Nikola Kavazovic, anatarajiwa kuchukua mikoba ya Cedric Kaze ndani ya kikosi cha Yanga.

 

Yanga ambayo hivi karibuni ilifikia uamuzi wa kulivunja benchi lake la ufundi kutokana na timu yao kupata matokeo mabaya kwa siku za karibuni, hivi sasa ipo kwenye mchakato wa kupata kocha mkuu mpya.Wakati mchakato huo ukiendelea, hivi sasa kikosi hicho kipo chini ya kocha wa muda, Juma Mwambusi.

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Yanga, Kavazovic raia wa Serbia, muda wowote anatarajiwa kutua ndani ya Yanga baada ya uongozi wa timu hiyo kuona ndiye anafaa.

 

“Baada ya kikao cha haraka cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika juzi usiku, kimefikia muafaka wa kumleta kocha huyo, mipango yote imefanyika kutokana na hali ya timu ambapo uongozi umepanga kutumia mapumziko haya kuirekebisha timu kwa kuipatia michezo mingi ya kirafiki.

 

“Kavazovic atakuja kuungana na kocha msaidizi mzawa ambaye tayari tumeshamtambulisha baada ya kufanya naye mazungumzo,” kilisema chanzo hicho.

 

Timu alizowahi kuzifundisha kocha huyo ni BASK (1996–2005), OFK Žarkovo (2006–2008), Borac (2008–2010), Resnik (2010–2012), FC Istiklol (2012–2013), Tajikistan (2012–2013), Sri Lanka (2014–2015), New Radiant (2015), Lanexang United (2016), New Radiant (2016), Saif (2016–2017), Township Rollers (2017–2018), AFC Leopards (2018), na Free State Stars (2018–2019).

STORI: MUSA MATEJA, DAR ES SALAAM

Leave a Comment