×

Tanzia: Mfalme wa Wazulu Afariki Dunia


Mfalme wa Wazulu wa Afrika Kusini, Goodwill Zwelithini amefariki katika Hospitali ya KwaZulu-Natal alipokuwa anatibiwa Kisukari.

Mfalme Zwelithini ameugua kwa takriban mwezi mmoja kabla ya umauti kumkuta alfajiri ya Machi 12. Amekuwa Mtawala wa Zulu tangu 1968.

Zwelithini ni Mfalme wa nane wa Wazulu ambapo alimrithi baba yake Mfalme Bhekuzulu kaSolomon.

Leave a Comment