
RAIS wa Uganda Yoweri Museveni amesema bado hajaruhusu wataalamu wa afya wampe chanjo ya Corona na wala Mkewe Janeth Museveni hajachanjwa hiyo chanjo ya Corona kwakuwa anataka chanjo hiyo waanze kupewa watu ambao wanaugua Corona ambao anaamini wana uhitaji zaidi.
Katika hotuba yake usiku wa kuamkia leo Machi 15, Rais Museveni amesema hajapata chanjo bado kwa kuwa yuko makini na ana ulinzi wa kutoka kwenye mfumo wa kiusalama, pia anaendelea kuangalia ni chanjo ipi ni nzuri zaidi kuitumia ”
Mwezi uliopita waziri wa afya wa nchini humo Jane Aceng , alikanusha taarifa kuwa rais na watu wake wa karibu walikuwa wanapokea chanjo nyingine kwa siri kabla ya taifa hilo kupokea chanjo rasmi.
Alitoa ufafanuzi baada ya gazeti la nchini humo la Daily Monitor na gazeti la Marekani la jarida la Wall Street.
Aidha rais Museveni amelitaka gazeti hilo kuomba radhi kwa kuandika barua kwenye kurasa ya mbele ya gazeti au atawafuata.