×

WHO Yamlilia Rais Magufuli

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus ni miongoni mwa watu waliotuma salamu za pole kufuatia kifo cha Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kilichotekea jana Jumatano Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam.

 

 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Ghebreyesus ameonyesha kuguswa na msiba huo mkubwa kwa Taifa la Tanzania na dunia kwa ujumla.

 

 

“Natuma salamu za pole kwa Serikali ya Tanznaia kufuatia kifo cha Rais John Magufuli tunaungana na familia na Taifa zima la Tanzania katika kuomboleza msiba huu na kuwafariji katika kipindi hiki kigumu.

 

 

Taarifa za kifo cha Rais Magufuli, zilitangazwa jana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisema Magufuli alifariki dunia saa 12 jioni kwa maradhi ya moyo baada ya kulazwa katika hospitali hiyo tangu Machi 6.

Leave a Comment