×

TANZIA: Rais wa Zamani wa Madagascar Didier Ratsiraka Afariki

RAIS wa zamani wa Madagascar Didier Ignace Ratsiraka amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84, rais wa nchi hiyo ametangaza.

“Jumapili tarehe 28 Machi, 2021, rais wa zamani, Admirali Didier Ignace Ratsiraka alifariki akiwa na miaka 84.

“Wamadagascar wamempoteza mzalendo,” Rais Andry Rajoelina aliandika katika Twitter.

 

Rais ametuma salamu za rambimbi kwa jamaa zake, jamii ya majeshi na raia wa Madagascar.

Rais huyo wa zamani alifariki katika hospitali ya kijeshi ya Soavinandriana iliyopo mji mkuu, Antananarivo, ambako alikua akipokea matibabi tangu tarehe 22 mwezi huu wa Machi.

 

Bw. Ratsiraka, ambaye aliingia madarakani akiwa afisa wa ngazi ya chini wa jeshi la majini mwaka 1975, aliongoza Madagascar mwaka 1991 na baadaye tena kuanzia mwaka 1996 hadi 2002.

Baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2002, aliondoka nchini humo na kwenda Ufaransa na kurejea nyumbani miaka tisa baadae.

 

Akiwa uhamishoni mwaka 2003, mahakama nchini Madagascar ilimhukumu kifungo cha miaka 10 gerezani bila kuwepo alipopatikanana kosa la ufisadi.

Miaka kadhaa baadae, rais wa sasa alimuachia huru na kumruhusu arudi nyumbani.

Leave a Comment