×

Serikali Yasema Itapitia Utaratibu wa Malipo ya Mikopo ya Elimu

Serikali imesema ipo katika mpango wa kupitia utaratibu wa malipo kwa wanufaika wa Mikopo ya Elimu ya Juu ili wapunguziwe mzigo.

 

 

Naibu Waziri wa #Elimu, Omari Kipanga, amesema hayo akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee, aliyehoji ni lini Serikali itapeleka mapendekezo ya #Sheria ili kuwaondolea mzigo wanufaika wa Mikopo kwani mpango huo umekuwa Biashara.

 

 

Halima Mdee amesema, Serikali inasema inawasaidia watoto wa masikini wakati inawaumiza kwa mlolongo wa madeni.”

Leave a Comment