×

Watumishi wa Tanesco Kizimbani kwa Tuhuma za Uhujumu Uchumi

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Arusha imewafikisha Mahakamani Watumishi watano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa tuhuma za Rushwa na Uhujumu Uchumi uliosababishia Serikali hasara ya Tsh. Milioni 387.

 

 

Wanaoshtakiwa ni Maria Mwakabage aliyekuwa Ofisa Ugavi na Usafirishaji Mwandamizi, Zipporah Ngadada na Ruthh Dedu waliokuwa Watunza Stoo, Florencia Nyambari na Michael Gumbo waliokuwa Watunza Stoo Wasaidizi.

 

 

Wanatuhumiwa kuwa kati ya mwaka 2016 na 2019 wakiwa Watumishi wa TANESCO Mkoani Arusha, walisababisha upotevu wa Mali za Shirika zenye thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 387, huku shtaka la pili likiwa ni kutumia nyaraka za uongo kumuhadaa Muajiri.

 

 

Watuhumiwa walisomewa mashtaka yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arusha.

 

 

Leave a Comment