×

Baraza la Ulamaa Lateua Masheikh 19 wa Mikoa

Baraza Kuu la Ulamaa la Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata) chini ya mwenyekiti wake, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir limefanya uteuzi wa masheikh wa mikoa 19.

 

 

Wajumbe wa baraza hilo walikaa jana Aprili 4, 2021 na kufanya uteuzi huo kwa mujibu wa katiba ya Bakwata. Uteuzi wa masheikh hao wa mikoa umetangazwa leo Jumatatu Aprili 5, 2021 na msemaji wa Mufti, Khamis Mataka.

 

 

Mataka aliwataja miongoni mwa masheikh wa mikoa walioteuliwa ni pamoja na Alhad Mussa Salum ( Dar es Salaam), Shaaban Juma (Arusha), Mustafa Rajab ( Dodoma) na Mohammad Mushangani wa Lindi.

 

 

Katika hatua nyingine, Sheikh Mataka amesema Mufti Zubeir amewateua wajumbe tisa wa baraza la Ulamaa ambao ni pamoja na Sheikh Hamid Jongo, Ally Khamis, Shaaban Msuya, Issa Othman na Mkowe Abdallah.

 

 

Msemaji wa samaha Mufti sheikh Khamisi Mataka amesema Baraza la Ulamaa katika kikao chake cha tarehe 04/04/2021 chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana kwa Mujibu wa Katiba ya BAKWATA ya Mwaka 1999 toleo la Mwaka 2018 ibara ya
63(6) limefanya uteuzi wa Masheikh wafuatao kuwa masheikh wa
Mikoa:-

 

MASHEIKH WA MIKOA

1. ARUSHA : SHABANI JUMA

2. KILIMANJARO : MLEWA SHABANI KIMWAGA

3. DAR ES SALAAM : ALHAD MUSA SALIM

4. DODOMA : MUSTAFA RAJABU

5. LINDI : MOHAMMED SAID MUSHANGANI

6. MANYARA : MOHAMMED KADIDI

7. MARA : MSABAHA KASIM NGABO

8. GEITA : ALHAD YUSUPH KABAJU

9. MTWARA : NURDIN MANGOCHI

10. SINGIDA : SHEIKH SALUM .M. MAHAMI

11. TANGA : ALI JUMA LUWUCHU

12. KAGERA : HARUNA KICHWABUTA

13. RUKWA : RASHID AKILIMALI.

14. TABORA : IBRAHIMU MAVUMBI.

15. NJOMBE : RAJABU MSIGWA

16. SIMIYU : MAHMOUD KALOKOLA

17. SHINYANGA : ISMAIL HABIBU MAKUSANYA

18. SONGWE : HUSSEIN BATUZA

19. Pwani : Abbasi Khamisi Mtupa

 

Masheikh hao wanaungana na
20. Sheikh Hassani Musa Kabeke wa Mwanza na
21. Sheikh Mashaka Nassoro Kakulukulu wa Katavi
ambao walishateuliwa awali.

 

Aidha katika kikao hicho Baraza la Ulamaa limewakaimisha masheikh wapya wa Mikoa ifuatayo:-

22. RUVUMA : ALLY MAHABA

23. MBEYA : MSAFIRI AYASI NJALAMBAHA

24. IRINGA : SHEIKH SAID AL ABRI

 

Aidha, taarifa hiyo imesema wafuatao wataendelea kukaimu nafasi zao mpaka pale Baraza la Ulamaa litakapofanya uteuzi rasmi kwa Mikoa hiyo.

25. Sheikh Twaha Kilango wa Mkoa wa Morogoro na
26. Sheikh Iddi Hassani Kiburwa

 

MAKATIBU WA MABARAZA YA MASHEIKH

Msemaji huyo wa mufti amesema Baraza la Ulamaa katika kikao chake cha tarehe 04/04/2021 chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana kwa Mujibu wa Katiba ya BAKWATA ya Mwaka 1999 toleo la Mwaka 2018 ibara ya 63(7) limefanya uteuzi wa Makatibu wa Baraza la Masheikh la Mikoa kama ifuatavyo:-

 

1. ARUSHA : SAID ABDALLAH CHUDI

2. KILIMANJARO : TAQDIR HAJJ MUHAMMED DHAHABU

3. DAR ES SALAAM. : ALLY SAID KIZEGERO

4. DODOMA. : BUNIAMINI ABASI ABDURABI

5. NJOMBE : USTADH. SAAD ALLY

6. MOROGORO : AJALI AHMED MLENGA

7. MWANZA : ALHAJI OTHMAN MASASI

8. LINDI:

9. MANYARA: UST. MWINYI MASOUD RASHID.

10. MARA : SALUM MOHAMED NYISUKA

11. GEITA : BAHARAN RAMADHANI SALUM

12. MTWARA : ABDULHAFIDH KASSIM

13. MBEYA : ABASI MSHAURI

14. SINGIDA : SHEIKH OMARY ABUBAKAR ALLY

15. TANGA : USTADH JUMA BAKARI

16. KAGERA : NAJIM MUSTAFA KHALID

17. KIGOMA : ALHAJI MAULID SANGI

18. IRINGA. : ABDULRAHIM NGOLE

19. PWANI : USTADH SALMIN AMMAR BUDAP

20. RUKWA : UST. MBEGU ABDALLAH HANGOLWA

21. SHINYANGA :
22. SIMIYU : HUSSEIN AHAMADI MBARUKU

23. KATAVI : SHEIKH MUSSA KHAMISI KAZIGE

24. TABORA : SHEIKH JABU SAID

25. RUVUMA :
26. SONGWE : SHEIKH ALLY MAMBEA

 

MAKADHI

Wakati huohuo Mheshimiwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana kwa Mujibu wa Katiba ya BAKWATA ya Mwaka 1999 toleo la Mwaka 2018 ibara ya 84(13) amefanya uteuzi wa Makadhi wa Mikoa kama ifuatavyo:-

 

1. ARUSHA : SHEIKH RAJABU HASSAN KIUNGIZA

2. KILIMANJARO : SHEIKH HUSSEIN HAMISI CHIFUPA

3. DAR ES SALAAM : RAMADHANI SALUMU OMAR KITOGO

4. DODOMA. : SHEIKH KISUSU BIN MKUMBO MWAGONDA

5. MOROGORO : SHEIKH MUSA HARUNA BORINGO.

6. MWANZA : SHEIKH HAMISI ALMASI

7. MANYARA : SHEIKH JUMA ISERE.

8. MARA : SHEIKH JUMA ADAMU

9. GEITA : SHEIKH ELIYASA SAID

10. MTWARA : SEIKH ABALLAH ALI HEMED

11. MBEYA : SHEIKH HASSAN MBARAZI

12. : SINGIDA : SHEIKH SHABANI CHAMBILA MKANGA

13. KAGERA : SHEIKH MAULANA MBARAKA JUMA

14. KIGOMA : SHEIKH IDRISA ABDULMUHSIN KITUMBA

15. IRINGA. : SHEIKH ABUBAKAR CHALAMILA

16. PWANI : SHEIKH ZUBEIR RASHID

17. RUKWA : SHEIKH KHAMISI ISSA KIGEZI

18. TABORA : SHEIKH IBRAHIMU HAJI

19. KATAVI : SHEIKH MAJALIWA MRISHO

20. NJOMBE : SHEIKH ABDALLAH SWALEHE ABDALLAH

21. SIMIYU : SHEIKH ISSA KWEZI KIDAI

22. SONGWE : SHEIKH IDD KASSIM

 

Taarifa hiyo imesema Mikoa Minne (4) iliyobakia uteuzi wake utafuatia baadae.

MAKATIBU WA MAKADHI WA MIKOA

 

Mheshimiwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana kwa Mujibu wa Katiba ya BAKWATA ya Mwaka 1999 toleo la Mwaka 2018 ibara ya 84 (13) amefanya uteuzi wa Makatibu wa Makadhi wa Mikoa kama ifuatavyo:-

1. ARUSHA : SHEIKH MBARAKA MUSA MTONYI

2. KILIMANJARO : USTADH ISSA JUMA ISSA.

3. DAR ES SALAAM : SHEIKH ABDULKARIM PAZI.

4. DODOMA. : MOHAMED SENDORO

5. MOROGORO : USTADH SWALEHE KASIM LUKANDA

6. MWANZA : USTADH RAMADHANI KHAMISI

7. MANYARA : USTADH ADAM ISSA ZUBEIR.

8. MARA : KUDRA IBRAHIM MIGOZI

9. GEITA : HAMISI MRISHO MLEA

10. MTWARA : MUSSA HAMISI MWARABU

11. MBEYA : ALLY KHAMIS FURUKUTU

12. SINGIDA : BDALLAH TAKAZA

13. KAGERA MIKIDADI ABASI BANOBI

14. KIGOMA : MAJALIWA AHMAD KAGAMA

15. IRINGA. : USTADH ABDALLAH KHALID

16. RUKWA : USTADH ABDALLAH HASAN KATALANGO

17. TABORA. : ATHUMANI BAKAR KABOGOTA

18. KATAVI : SHEIKH OMAR SHABANI KABWIRI

19. NJOMBE : IDD AMANI GADAU

20. SIMIYU : KASSIM RAJABU MOHAMED

21. SONGWE : HUSSEIN JUMA

22. TANGA : USTADH ALLY SALEH

 

Mazungumzo hayo nawaandishi wa habari yaliyofanyika leo mchana mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam yalihudhuriwa pia na katibu mkuu BAKWATA alhaj Nuhi Mruma pamoja na katibu wa mufti sheikh Mussa Hemedi.

 

Harith Nkussa
Mwandishi Maalum wa Mufti
Jumatatu 5.4.2021
Ubayudi, Bolisa, Kondoa

Leave a Comment