×

Rais Magufuli Alivyoagiza Mkurugenzi TPDC Arejeshwe Kazini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli (wakati huo) aliagiza Dkt. James Mataragio arejeshwe katika nafasi yake ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), baada ya kusimamishwa kazi tangu Agosti 2016.

 

 

Agizo hilo alilitoa Julai 22, 2019 kupitia taarifa ya Ikulu ambayo imeeleza kuwa Rais, ameitaka Wizara ya Nishati kumrejesha kazini Mkurugenzi huyo Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania.

 

 

Ikumbukwe kuwa, jana Jumapili, Aprili 4, 2021, Rais wa sasa Mama Samia Suluhu Hassan alifanya mabadiliko ya makatibu wakuu, wakurugenzi na baadhi ya wakuu wa Idara za Serikali ambapo miongoni mwao, Dkt. Mataragio aliondolewa katika nafasi hiyo na kuteuliwa ndugu Thobias Mwesigwa kushika wadhifa huo, lakini leo Jumatatu asubuhi, Mama Samia amemrejesha Dkt. Mataragio katika nafasi yake na kutengua uteuzi wa Mwesigwa.

 

Leave a Comment