
BAADA ya Azam FC, kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa na kukaa nafasi ya pili, kocha mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina amesema watapambana kuisaka nafasi ya kwanza inayokamatiwa na Yanga.
Yanga ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara, kabla ya mchezo wa jana dhidi ya KMC, walikuwa na pointi 50.
Azam ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 47 ikicheza mechi 25, huku Simba ikiwa ya tatu na pointi zake 44 kutokana na mechi 20.
Akizungumza na Spoti Xtra, Lwandamina alisema: “Kwa sasa tutahakikisha tunafanya vizuri zaidi ili kupanda juu kwenye msimamo, hatubweteki kwa nafasi ya pili tuliyonayo, tunataka kuwa wa kwanza, waliopo hapo wametushikia.”
JOEL THOMAS, Dar