×

Urusi Yatimua Wanadiplomasia 10 wa Marekani

URUSI imewataka wanadiplomasia 10 wa Marekani kuondoka nchini humo katika hatua ya kulipiza kisasi baada ya Marekani kuwafukuza wanadiplomasia 10 wa Urusi kwa madai ya udukuzi na kuingilia uchaguzi wa Marekani.

 

Urusi imewataka wanadiplomasia 10 wa Marekani kuondoka nchini humo katika hatua ya kulipiza kisasi baada ya Marekani kuwafukuza wanadiplomasia 10 wa Urusi kwa madai ya udukuzi na kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka uliopita.

 

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema John Sullivan, ambaye ni balozi wa Marekani nchini Urusi, anapaswa kurudi nyumbani katika kile walichosema ni kwa mashauriano zaidi.

 

Kupitia taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema huu ni wakati wa Marekani kuonyesha ukomavu wake wa kiakili na kugeuza mkondo wao wa kugombana.

 

Taarifa hiyo imeongeza kusema kuwa ina uwezo wa kuiumiza zaidi Marekani kuichumi na kupunguza idadi ya wanadiplomasia wa Marekani nchini Urusi hadi 300, japo kwa sasa haitachukua hatua hiyo.

 

Leave a Comment