





IKIWA sasa ni msimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo waislam wako katika mfungo, timu ya masoko ya Kampuni ya Global Publishers, leo Jumamosi, Aprili 18,2021 imemwaga fedha mara mbili ya aliyonunulia msomaji wa gazeti la Championi kama ofa kwa waliokutwa wanasoma Gazeti la Championi Jumamosi ambalo uchapishwa na kampuni hiyo ikiwa ni mahususi kwa Habari za michezo.
Wasomaji mbalimbali waliokuwa wakisoma gazeti hilo ambalo hutoka kila siku ya Jumamosi, wamerudishiwa fedha zao walizotumia kununua gazeti hilo. Promosheni hiyo ilifanyika maeneo mbalimbali jijini Dar.
Wasomaji hao walionekana kufurahia ofa hiyo ambayo itakuwa endelevu hususani katika msimu huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Wiki ijayo una nafasi ya wewe msomaji kurudishiwa fedha pia utakayotumia kununulia Gazeti la Championi Jumamosi linalouzwa Sh 800, kama utakutwa na timu ya masoko ukiwa unasoma gazeti hilo.