×

Samia: Tumepitia Kipindi Kigumu Baada ya Magufuli Kufariki

 

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, wabunge na Watanzania akisema kifo cha rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli kiliifanya nchi kupitia kipindi kigumu cha historia ya uongozi.

 

 

Ameeleza hayo leo Alhamisi Oktoba 22, 2021 wakati akilihutubia Bunge la Tanzania ikiwa ni hotuba yake ya kwanza tangu kuapishwa kushika wadhifa huo Machi 19, 2021.

 

 

“Napenda kutoa pole nyingi kwa familia hususan mama mzazi wa marehemu, Suzana Magufuli na mke wa marehemu, Janeth Magufuli, watoto, ndugu jamaa napenda kutoa pole kwa wabunge kwani alikuwa mbunge mwenzenu kwa miaka 20 na kama mnavyofahamu Rais ni sehemu ya Bunge.”

 

 

“Nawapa pole nyingi Watanzania wote kwa kumpoteza kiongozi huyu ambaye tulimpenda na tunathamini mchango wake kwa taifa,” amesema.

 

 

Rais Samia alilisimamisha Bunge kwa dakika moja kabla ya kuanza hotuba yake ikiwa ni ishara ya kumkumbuka kiongozi huyo ambaye alisema kuwa alikuwa na jasiri i mwenye maono ambaye aliipenda nchi yake na kuitumikia.

Leave a Comment